VIDEO: Mbunge Bulaya apewa mikoba ya Tundu Lissu

Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya akiwa ndani ya ukumbi wa bunge baada ya kutangazwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwa amechaguliwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kuwa mnadhimu mkuu wa kambiu hiyo, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Bunge la Tanzania limemtangaza Mbunge wa Bunda (Chadema), Ester Bulaya kuwa mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Dodoma. Bunge la Tanzania limemtangaza Mbunge wa Bunda (Chadema), Ester Bulaya kuwa mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Leo Jumanne Januari 28, 2020 Spika Job Ndugai amemtangaza Bulaya akibainisha kuwa amepokea jina hilo kutoka kwa kiongozi wa kambi hiyo bungeni, Freeman Mbowe.

Bulaya anachukua nafasi ya aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyevuliwa ubunge kwa madai ya kutoonekana bungeni bila taarifa yoyote.

Kabla ya uteuzi huo wa Bulaya, mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alikuwa anakaimu nafasi hiyo. Selasini alijiuzulu wiki iliyopita.

Mbali na kumtangaza Bulaya, Spika Ndugai amempongeza Mbowe kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine kuwa mwenyekiti wa Chadema na John Mnyika kuwa katibu mkuu wa chama hicho.

SOMA ZAIDI: