Mbunge awarushia kombora wataalamu wanao kagua miradi, asema wanavioja

Tuesday November 5 2019

By Habel Chidawali, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Mbunge wa Sikonge (CCM), Joseph Kakunda amesema kuna vioja katika ukaguzi wa miradi na wanaotakiwa kubebeshwa lawama ni wataalamu.

Kakunda ametoa kauli hiyo leo Jumanne Novemba 5,2019 wakati akichangia mapendekezo ya mpango wa maendeleo ya Taifa na mwongozo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2020/21.

Kakunda ambaye amewahi kuhudumu katika nafasi ya Waziri wa Viwanda, amesema wataalamu wa Tanzania wengi wamejikita kutembelea miradi siyo kuikagua.

Amesema iko tofauti kubwa kati ya kukagua viwanda na kutembelea viwanda lakini kinachoshangaza ni wataalamu nao kuamua kuwa watembeleaji wa viwanda.

“Kuna vioja sana kwa wataalamu wetu, wanashindwa kukagua miradi badala yake nao wanakuwa sehemu ya watembelea miradi, hii si sawa hata kidogo, lazima wabadilike,”  amesema Kakunda.

Mbunge huyo amewataka wataalamu kabla ya kutembelea miradi wawe na mikataba ya miradi wanayoitembelea ili waone namna ya kuisimamia kwa mapana kwa kufuata mikataba.

Advertisement

Katika hatua nyingine, mbunge huyo amesema ni wakati sasa kwa Serikali kuhakikisha kila kipande cha Tanzania kiwe kimepimwa ili kuboresha uwekezaji kwa kuwa ardhi ndiyo chanzo kikuu cha uwekezaji.

Advertisement