Mchakato wa kumng’oa Trump sasa rasmi

Muktasari:

Bunge la Marekani lasafisha njia kumshtaki baada ya kupiga kura kuidhinisha kutumwa kwa mashtaka kwenda katika Baraza la Seneti ili kuanza kwa kesi ya kumng’oa madarakani.

T. Mchakato wa kumng’oa Trump sasa rasmi

S. Bunge la Marekani lasafisha njia kumshtaki baada ya kupiga kura kuidhinisha kutumwa kwa mashtaka kwenda katika Baraza la Seneti ili kuanza kwa kesi ya kumng’oa madarakani.

Washington, Marekani. Baraza la Wawakilishi nchini Marekani limepiga kura kuidhinisha kutumwa kwa mashtaka dhidi ya Rais Donald Trump kwenda katika Baraza la Seneti ikiwa ni hatua ambayo inaashiria kuanza kwa kesi inayoweza kumuondoa madarakani.

Hatua hiyo imekuja jana katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja tangu wabunge wa baraza hilo kumkuta na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia juhudi za bunge kuchunguza vitendo vyake.

Wabunge wa Baraza la Wawakilishi jana wamepitisha azimio hilo kwa kura 193 kati ya 228 zilizopigwa.

Baaada ya upigwaji wa kura hiyo, Spika Nancy Pelosi alisaini uamuzi huo sambamba na timu ya wabunge wa Democratic ambao wataendesha mashitaka ya kesi hiyo.

Vilevile, Spika Pelosi pia aliteua mameneja ambao watakuwa na jukumu la kuendesha mashitaka hayo.

Hata hivyo, Baraza la Seneti ambalo linadhibitiwa na chama tawala kinachoongozwa na Rais Trump litaamua ama kumtia hatiani kiongozi huyo na kumuondoa madarakani au kutoendelea na mashitaka hayo jambo ambalo halitarajiwi.

Katika mkutano na wanahabari kabla ya kutia saini kupelekwa kwa mashitaka hayo, Spika Pelosi alisema “leo tutaweka historia tutakapo peleka hati za mashitaka dhidi ya Rais wa Marekani kwa vitendo vyake vya matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia majukumu ya bnunge kushughulikia suala hilo.”