VIDEO: Mdee ataka wabunge wote wapimwe corona

Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee, akichangia bungeni jijini Dodoma leo baada ya Spika wa Bunge kutoa taarifa kwa wabunge ya mabadiriko ya uendesha wa vikao vya Bunge kutoka na ugonjwa wa virus vya corona. Picha na Anthony Siame

Muktasari:

  • Mbunge wa Kawe nchini Tanzania (Chadema), Halima Mdee ameshauri wabunge wote kupimwa virusi vya corona ili kufahamu afya zao badala ya inavyofanyika hivi sasa ya kupima joto la mwili la kila mtu anayeingia kwenye viwanja vya Bunge

Dodoma. Mbunge wa Kawe nchini Tanzania (Chadema), Halima Mdee ameshauri wabunge wote kupimwa virusi vya ugonjwa wa corona na wale watakaobainika wakawekwe katika karantini.


Halima ameyasema hayo leo Jumanne Machi 31 2020, mara baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai alipotoa taarifa ya hatua zilizochukuliwa na Bunge katika kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.


Ametaka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto kutoa taarifa bungeni ya kina ya hali ya corona nchini na hatua zinazochukuliwa katika kukabiliana na ugonjwa huo.


Amesema ukaaji wa mbalimbali baina ya mtu na mtu, upo kwa watu wenye kipaumbele (privilege) na watu wenye uwezo wa kati lakini sio huko mitaani, daladala na kwenye mwendokasi.
Amesema pia wizara hiyo iseme kuwa ina mpango gani wa kibajeti kwasababu katika nchi nyingine dunia wakiamua kujitenga wanawafidia wafanyabiashara.


“Sasa kama leo Serikali inaweza kuperfom kwa only (tu) asilimia 15 tu ya total bajeti kwenye wizara muhimu kama ya afya hivi corona can we manage? Kwa hiyo tukija kuzungumza tunaweza kuishauri vizuri Serikali ,”amesema na kuongeza.


"Leo wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi inabidi tusambazwe huko labda tungepimwa ili ijulikane kama Halima ana corona nipelekwe kwenye karantini ili wabaki watu wafanye kazi lakini wabunge leo wapo kwenye vyumba lakini kwanini tusianze na sisi tupimwe wote.”


Amesema kama nchi kuna hatua zanakuchukuliwa lakini bila kuwa na  taarifa za uhakika hawawezi kujadili na kuokoa watu wao.