VIDEO: Mdee amwaga chozi

Mwenyekiti wa Baraza la wanawake chadema (Bawacha), Halima Mdee akifuta machozi wakati akiwashukuru wananchi waliojitolea kuwachangia viongozi wa chama hicho ambao walihukumiwa kulipa faini ya sh 350 milioni. Picha na Ericky Boniphace

Dar es Salaam. Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akizungumza na wanahabari leo Alhamisi, Machi 12, 2020 baada ya kutoka gereza la Segerea amesema Watanzania wameonyesha imani kubwa kwa Chadema.


"Nawashukuru sana Watanzania, walijua hatuna fedha, ni kweli hatukuwa na pesa kabisa, walijua mapema tunaenda jela," amesema Mdee huku akimwaga machozi hatua iliyofanya wengine kuangua kilio.


"Walishafunga akaunti zote mwenyekiti wetu Mbowe, wamemfilisi, wakaanglia sisi wengine hali zetu tusingeweza kulipa fidia hizo.”