Mdogo wa Kanumba Seth Bosco afariki dunia

Muktasari:

Seth Bosco ambaye ni mdogo wa marehemu Steven Kanumba, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumamosi baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani kwa mama yake Mbezi jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.


Dar es Salaam. Seth Bosco ambaye ni mdogo wa aliyekuwa mwigizaji maarufu nchini Tanzania marehemu Steven Kanumba amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumamosi Desemba 7, 2019.

Kwa takribani miezi mitatu Bosco ambaye pia ni muigizaji nchini Tanzania alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kupooza.

Kwa mara kadhaa mama Kanumba, ambaye ni mama yake mkubwa aliyekuwa akimuuguza, alipohojiwa na vyombo vya habari alisema msanii huyo alikuwa akisumbuliwa na uvimbe kwenye mgongo.

Taarifa ya kifo chake zimethibitishwa na  Chama cha Waigizaji Kinondoni, Dar es Salaam nchini Tanzania.

Katika taarifa ya chama hicho  iiliyotolewa  na kusainiwa na Ofisa habari wake, Masoud Kaftany, imesema Bosco amefariki usiku wa kuamkia leo nyumban kwao Mbezi Temboni.

Kaftany amebainisha kuwa msiba upo mbezi kwa Mama Kanumba na

taratibu zingine watu wutajulishwa ikiwamo ratiba za mazishi.

Steven Kanumba ambaye ni kaka wa Seth alifariki Aprili 7,2012

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi