Menina aitwa Basata kuhojiwa

Friday October 11 2019

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limemtaka msanii Menina Attick  maarufu Meninah kuripoti katika ofisi zake zilizopo Ilala, Dar es Salaam.

Wito huyo wa Basata unatokana picha za utupu zinazodaiwa kuwa za msanii huyo kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Oktoba 11, 2019 baada ya kuulizwa kuhusu barua ya wito ya Baraza hilo kwenda kwa Menina, katibu mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza amesema wamemuita kutokana na kinachosambazwa mitandaoni.

“Ndiyo tumemuita kwa ajili ya mahojiano, tunataka kufahamu alikuwa anafanya mambo hayo kwa sababu gani maana elimu imekuwa ikitolewa mara kwa mara lakini mambo yanajirudia,” amesema Mngereza.

 

 

Advertisement

 


Advertisement