Meya wa Iringa aitwa kikaoni kesho

Wednesday March 25 2020

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Iringa. Baraza la madiwani Iringa mjini litakutana kesho Machi 26, 2020 huku kukitarajiwa maamuzi ya kumvua umeya, Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe.

Barua iliyotolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa hiyo, Hamid Njovu kwenda kwa Kimbe imemtaka kufika bila kukosa.

Machi 2 mwaka huu Kimbe alikiri kupokea barua kutoka kwa Njovu akitakiwa kujibu tuhuma zinazomkabili ndani ya siku tano.

Kimbe alisema anakabiliwa na tuhuma za mashtaka manne  ambayo ni matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya rasilimali za halmashauri, mwenendo mbaya au ukosefu wa adabu na kushiriki vitendo vya rushwa.

Kimbe kupitia akaunti yake ya Twitter ameeleza kuwa alifungua kesi mahakamani kupinga hatua zinazochukuliwa na baraza la mawaziri na hukumu ilitakiwa kutoka Machi 27 ila ameshangazwa na kesho kuitwa kikaoni

Advertisement