FAHAMU: Huyu ndiye Salum Shamte

Salum Shamte, aliyefariki jana asubuhi akiwa na miaka 69, ameacha sifa kama mtu ali-yechangia kufufua zao la mkonge na aliyepigania sekta binafsi.

Shamte alizaliwa Julai 10, 1951 mjini Tabora ambako baba yake alikuwa akifanyia kazi kwenye Shirika la Reli. Elimu ya msingi aliipata katika Shule ya Msingi Nawenge iliyopo Mahenge mkoani Morogoro na kujiunga na sekondari mjini Shinyanga kabla ya kusoma elimu ya juu ya sekondari Shule ya Pugu.

 Shahada ya masuala ya uchumi wa kilimo aliipata Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya. Pia alikuwa na shahada ya uzamivu ya uongozi wa biashara. Shamte, ambaye anatarajiwa kuzikwa leo, ni jina kubwa katika sekta ya kilimo na biashara akishiriki katika kilimo kwa zaidi ya miaka 44.

Pia katika miaka 10 ya maisha yake aliwahi kufanya kazi nchini Uingereza akisimamia soko la katani. Mwishoni mwa mwaka 2017, Shamte aliachia ngazi kama mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Katani. Kampuni hiyo imejikita katika masuala ya kilimo na uchakataji wa katani.

Pia inajishughulisha na kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao la katani. Pamoja na kutengeneza bidhaa hizo, pia inaendesha shughuli za kuzalisha nishati kutokana na mazao ya mkonge. Shamte, ambaye ameacha watoto

wanne wa kiume na wata-no wa kike, alikuwa amebobea katika kilimo cha embe, mpunga na ufugaji wa kuku na samaki.

Aliwahi kuwa mwenyekiti wa Baraza la Kilimo la Tanzania (ACT) kuanzia mwaka 2006 hadi 2013. Katika kipindi hicho, ACT ilihusi-ka kwa kiasi kikubwa katika kuasisi programu ya Kilimo Kwanza waka