Mitandao inavyowaweka kitanzini wasanii nchini Tanzania

Muktasari:

Wataalamu wa saikolojia na wakongwe wa burudani wamesema wimbi la wasanii kukosa maadili limetokana na Serikali kupuuza utoaji wa elimu ya utamaduni kwa shule za msingi kuanzia mwaka 1995.

Dar es Salaam. Wataalamu wa saikolojia na wakongwe wa burudani wamesema wimbi la wasanii kukosa maadili limetokana na Serikali kupuuza utoaji wa elimu ya utamaduni kwa shule za msingi kuanzia mwaka 1995.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu Tanzania ishuhudie uvunjifu wa maadili kwa wasanii, ikiwemo kukiuka sheria za nchi hali na kusababisha wengi kuitwa polisi na baadhi kufikishwa mahakamani na katika taasisi za utamaduni kuhojiwa.

Mtaalamu wa saikolojia na mwandishi wa vitabu, Charles Nduku anataja changamoto mbili zinazowafanya wasanii wafanye makosa ya kujirudia kuwa ni kutozingatia usiri na mwitikio na mapokeo ya hadhira (emotional intelligence).

Nduku alisema mambo hayo mawili yamekuwa tatizo kwa wasanii wengi na Serikali ikishirikiana na taasisi, inapaswa kutoa elimu kwa kundi hilo ili kukomesha tatizo hilo.

“Changamoto ya kwanza kwenye emotional intelligence ni kujua athari ya maneno unayoyaweka kwenye wimbo, maneno au picha unayoitumia mtandaoni, kwanza kwake yeye na kwa hadhira anayoipelekea,” alisema.

Alitoa mfano wa sakata la Idris Sultan kuwa na mvutano wa pande mbili, uliosababishwa na mhusika kutozingatia nini anakipeleka kwenye hadhira na madhara kwa pande zote.

 

 

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumamosi Novemba 2, 2019