VIDEO: Mke wa Gwajima aeleza anavyomuamini mumewe

Hii ni picha ya familia na nilipiga na mke wangu huyu hapa

Muktasari:

Grace, mke wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amezungumzia kuhusu video ya ngono inayomuonyesha mtu mwenye sura kama ya mumewe, akisema si yeye kwa kuwa anamfahamu vyema

Dar es Salaam. Siku moja baada ya kusambaa kwa video ya ngono ikimuonyesha mtu mwenye sura inayofanana na ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa faragha na mwanamke ambaye bado hajafahamika, Grace mke wa kiongozi huyo wa kiroho amevunja ukimya.

Akizungumza leo Jumatano Mei 8, 2019 jijini Dar es Salaam wakati Gwajima akitoa ufafanuzi mbele ya wanahabari kuhusu video hiyo na kueleza kuwa si yake, Grace amesema anafahamu ukweli wa video hiyo na kamwe haiwezi kumyumbisha kwa maelezo kuwa anamfahamu vyema mumewe.

“Mimi ni kama simba, ukweli naufahamu, namfahamu mume wangu na kumuamini na ukweli huo hakuna mtu anayeweza kuubadilisha.”

“Nipo pamoja na yeye na nitasimama na yeye. Mungu akiwa upande wetu hakuna atakayeweza kuwa juu yetu,” amesema Grace.

Wakati Grace akizungumza mamia ya waumini wa kanisa hilo walionekana wakimshangilia na kuruka ruka kwa furaha.