Mke wa bilionea aliyeuawa Kenya aomba aruhusiwe kumzika mumewe

Saturday September 21 2019

 

Nairobi, Kenya. Sarah Waimuru  ambaye ni mke wa bilionea maarufu nchini Kenya, Tob Cohen amewasilisha ombi la kutaka mahakama imruhusu kushiriki shughuli za mazishi ya mumewe.

Bilioneaa Cohen ambaye alitoweka katika mazingira ya kutatanisha aliuawa na watu wasiyofahamika kisha mwili wake kutupwa katika tanki la maji nyumbani kwake anatajajiwa kuzikwa Jumatatu Septemba 23.

Mazishi ya bilionea Cohen yanatarajiwa kufanyika jijini Nairobi kwa mila za Kiyahudi na kuhudhuriwa na watu wa karibu wa familia hiyo akiwamo dada wa mfanyabishara huyo Gabrielle Van na mumewe.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mke wa bilionea huyo kukubalina na familia yake kumzika Jumatatu ijayo.

Polisi nchini Kenya inamshikilia mke wa bilionea huyo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mumewe kwa madai kuwa alipanga njama kwa kushirikiana na watuhumia wengine.

Awali kupitia kwa wakili wa mjane huyo ambaye kwa sasa yupo gereza la wanawake la Lisitata jijini Nairobi kwa tuhuma za kumuua mumewe jana alitoa tamko kuwa hatamruhusu mtu mwingine yeyote kumzika mume wake.

Advertisement

Katika barua hiyo ya wakili wake anayeitwa Philip Murgor, mke huyo alisema kwamba anajitambua kuwa yeye bado ni mke halali wa bilionea huyo na kwamba mwili huo usitolewe kwa dada yake anayeitwa Gabrielle.

Baada ya pingamizi hilo, mahakama ilitoa idhini na kutiwa saini na mawakili wa pande hizo mbili akiwamo dada wa Sarah na Gabrielle ambaye ni dada wa bilionea huyo walikubaliana kuzika nchini humo kwa.

Familia hizo zilikubaliana mambo matatu ya msingi ikiwamo, mwili wa bilionea huyo kuzikwa kwa mujibu wa mila ya Kiyahudi. Bilionea Cohen alikuwa raia wa Uholanzi.

Makubaliano hayo pia yameeleza kuwa sherehe ya mazishi hayo yatakuwa ya faragha na ya familia tu ambako Sarah atashiriki kama mjane.

Inaelezwa kuwa ibada ya mazishi itakuwa kwa mujibu wa ibada za Kiyahudi na viongozi wa jamii inayohusika wakati mazishi yatafanyika kwenye kaburi la Wayahudi kwenye Barabara ya Wangari Mathai saa 2 usiku.

Advertisement