Mmorocco aongeza machungu ya timu za nyumbani

Muktasari:

Jumamosi, Al Ahly ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Wydad Casablanca katika mechi nyingine ya kwanza ya nusu fainali za Ligi ya Mabingwa wa Afrika iliyofanyika Morocco, mabao yakifungwa na Mohamed 'Afsha' Magdy na Ali Maaloul.

Johannesburg, Afrika Kusini. Mchezaji wa Morocco, Achraf Bencharki jana Jumapili alikamilisha wiki ya balaa kwa klabu za nchi yakealipoifungia Zamalec bao pekee lililowazamisha wenyeji Raja Casablanca katika mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Jumamosi, Al Ahly ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Wydad Casablanca katika mechi nyingine ya kwanza ya nusu fainali za Ligi ya Mabingwa wa Afrika iliyofanyika Morocco, mabao yakifungwa na Mohamed 'Afsha' Magdy na Ali Maaloul.  

Ahly, wanaoshikilia rekodi ya kutwaa ubingwa wa Afrika mara nane na vigogo wenzao Zamalek, watakuwa wenyeji wa mechi za marudiano zitakazofanyika Misri Oktoba 23 na 24, kukiwa na uwezekano wa klabu zote za Misri kufuzu kucheza fainali.

Tangu michuano hiyo mikubwa Afrika ianzishwe mwaka 1964 haijawahi kutokea mechi ya fainali kukutanisha timu za nchi moja.

Kocha wa Raja, Jamal Sellami alilazimika kuteua kutoka idadi ya wachezaji wake 1kwa ajili ya mechi, bila ya kuwepo wachezaji watano tegemeo kutokana na watatu kati yao kuwa majeruhi na wawili kugundulika kuwa wana maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19.

Mlipuko wa ugonjwa huo ulimaanisha kuwa mechi zote mbili za nusu fainali zichezwe bila ya kuruhusu mashabiki katika uwanja wa Mohamed V wenye uwezo wa kuchukua watu 60,000 katika jiji hilo la kuibiashara nchini Morocco.

Bao la ushindi lililofungwa katika dakika ya 18 lilitokana na pasi ya kulenga kutoka kwa Ahmed 'Zizo' Sayed iliyopita nyuma ya kipa wa Raja, Anas Zniti na kudondokea kichwa kwa Bencharki aliyefunga kwa kuusukuma mpira kwa nguvu.

Bencharki, 26, alijiunga na Zamalek, ambao wameshatwaa ubingwa wa Afrika mara tano, mwaka jana akitokea klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia baada ya kuichezea Lens ya Ufaransa kwa mkopo.