Mpamba video za wasanii, mwenzake mahakamani kwa kujipiga picha za ngono

Monday February 17 2020

 

By Hadija Jumanne, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Aisha Juma (19) ambaye ni mpamba video za wasanii (video vixen) nchini Tanzania  na mwenzake wameikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka   ya kusambaza picha za ngono katika mitandao ya kijamii na kulawiti.

Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara, Samwel Philemon (34) mkazi wa Kigamboni.

Wamefikishwa mahakamani leo Jumatatu Februari 17, 2020 na  kusomewa kesi ya jinai namba 24/2020 mbele ya Hakimu Mkazi, Rashid Chaungu.

Wakili wa Serikali, Kija Luzungana amedai Desemba 12, 2019 jijini Dar es Salaam, Aisha anadaiwa  kusambaza picha za ngono kinyume na sheria ya mtandao.

Kija amedai  shtaka la pili la kulawiti linamkabili Philemon anayedaiwa siku ya tukio alimuingilia Aisha kinyume na maumbile na kujipiga picha, kisha kuzisambaza wakati akijua kuwa ni kinyume cha sheria.

Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yao walikana na upande wa mashtaka kudai upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Advertisement

Hakimu Chaungu ametoa masharti ya dhamana akiwataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za Serikali za mitaa, wanaotambulika kisheria watakao saini bondi ya Sh10 milioni.

Washtakiwa wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo kuahirishwa hadi  Februari 26, 2020.

Advertisement