Msafara wa magari ya kijeshi washambuliwa Uturuki

Picha na AFP

Muktasari:

Msemaji wa waasi wa National Liberation Front, Naji Mustafa alisema msafara huo ulikuwa ukielekea katika moja ya vituo vyake vya uchunguzi na ulinzi.

T. Msafara wa magari ya kijeshi washambuliwa Uturuki

S. Msemaji wa waasi wa National Liberation Front, Naji Mustafa alisema msafara huo ulikuwa ukielekea katika moja ya vituo vyake vya uchunguzi na ulinzi.

Syria. Majeshi ya Syria yameshambulia msafara wa magari ya kivita ya Uturuki na kusababisha vifo vya raia watatu.

Kwa mujibu wa Serikali ya Uturuki, msafara huo wa kijeshi ulikuwa ukielekea katika eneo linalotawaliwa na waasi Kaskazini mwa Syria.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Uturuki ilisema kwamba shambulio hilo lilitokea jana Jumatatu Agosti 19 katika Mkoa wa Idlib lilisababisha watu wengine 12 kujeruhiwa.

Msemaji wa waasi wa National Liberation Front, Naji Mustafa alisema msafara huo ulikuwa ukielekea katika moja ya vituo vyake vya uchunguzi na ulinzi.

Mwandishi wa Shirika la habari la AFP alisema kuwa alishuhudia msafara huo anasema ukiwa na magari 50 ya kijeshi na matano kati yao yakiwa vifaru.

Mkoa wa Idlib ni moja ya maeneo machache yasiodhibitiwa na Serikali ingawa ilitarajiwa kulindwa na kuwa eneo huru linalotenganisha majeshi ya upinzani.

Kwa muda mrefu eneo hilo limeshughudiwa mapigano na kusababisha mamia ya raia kuuawa hali inayochangia kuongezeka kwa hofu kubwa.

''Hii ndio hatari inayotukabili kwa sasa'', alisema Jan Egeland kutoka baraza la wakimbizi la Norway akizungumza na BBC.

Hata hivyo, Uturuki inayounga mkono baadhi ya waasi imeweka majeshi katika mji huo kama sehemu ya makubaliano na Urusi walipokutana mwaka uliopita.