Mtoto wa miezi miwili apona corona

Muktasari:

Mtoto huyo alilazwa hospitalini na mama yake aliyekuwa akiugua homa ya ini na wote wameshapona na kuruhusiwa kutoka.

Rome, Italia. Mtoto wa miezi miwili, ambaye inaaminika kuwa ndiye mgonjwa wa virusi vya coronamwenye umri mdogo kuliko wote nchini Italia, ameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kupona, vyombo vya habari vimeripoti.
Joto la mwili wa mtoto huyo halikuendelea kupanda na wala hakuwa na homa na aliruhusiwa na mama yake, ambaye amepona homa ya ini, ripoti hizo zimeeleza.
Wawili hao walilazwa katika hospitali iliyo jiji la Bari lililo kusini mwa Italia Machi 18.
Hadi jana, Italia ilishakuwa na vifo zaidi ya 17,600, idadi ambayoni kubwa kuliko nchi nyingine yoyote.
Serikali kwa sasa inafikiria ni lini na kwa jinsi gani itaondoa agizo la kuzuia watu kukaribiana iliyosaidia kupunguza kasi ya ongezeko la vifo vya kila siku kutoka vifo 969 kwa siku mwezi uliopita.