Mtunza fedha benki ya Exim adaiwa kuiba Sh120 milioni, akamatwa

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma  Gilles Muroto leo akuonyeshe sehemu ya fedha zilizobwa katika banki ya Exim tawi la Dodoma Agosti 28,2019. Picha na Nazael Mkiramweni

Muktasari:

Martin Temu (33), mtunza fedha wa Benki ya Exim tawi la Dodoma anashikiliwa na polisi kwa madai ya kuiba Sh120 milioni.

Dodoma.  Martin Temu (33), mtunza fedha wa Benki ya Exim tawi la Dodoma anashikiliwa na polisi kwa madai ya kuiba Sh120 milioni.

Akizungumza leo Ijumaa Oktoba 11, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema mtuhumiwa ni mkazi wa Dodoma, alipoiba fedha hizo alitoroka.

Amesema msako ulifanyika na alikamatwa mkoani Singida katika nyumba ya kulala wageni.

"Tulimkamata akiwa na Sh37.5 milioni kati ya fedha alizoiba,  mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili,” amesema Muroto.