Muroto asimulia waendesha bodaboda walivyozingira kituo cha polisi Dodoma

Wednesday September 11 2019

 

By Nazael Mkiramweni, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia waendesha bodaboda 70 kwa madai ya kuvamia kituo cha polisi kati mkoani humo na kufanya fujo wakishinikiza kutolewa mtuhumiwa aliyekuwa mahabusu ili wamuadhibu.

Mtuhumiwa huyo, Bazil Mjungu alikamatwa na polisi  kwa madai ya kusababisha ajali baada ya kumgonga dereva bodaboda.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Septemba 11, 2019 na

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto akibainisha kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 8, 2019.

Amesema waendesha bodaboda hayo waliamuriwa kutawanyika  lakini walikaidi amri hiyo na kuanza kufunga barabara, kuzingira kituo cha polisi kwa nia ya kukivamia.

"Walitawanywa kwa kufyatua risasi hewani lakini bado baadhi waliendelea kukaidi, hivyo watuhumiwa 20 walikamatwa na kufikishwa mahakamani  na kusomewa mashtaka ambapo walipatikana na hatia hivyo kuhukumiwa kifungo  cha miezi sita jela kila mmoja bila faini,” amesema Muroto.

Advertisement

Advertisement