Mvua yaleta adha ya usafiri Dar

Thursday October 17 2019

Maji ya  mvua iliyonyesha leo jijini Dar es

Maji ya  mvua iliyonyesha leo jijini Dar es Salaam yakiwa yamejaa kwenye barabara ya Pamba 

By Waandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimesababisha adha kwa watumiaji wa barabara katika maeneo mbalimbali jijini humo.

Leo Alhamisi Oktoba 17, 2019 mvua imeanza kunyesha asubuhi huku makamanda wa polisi wakieleza kuwa hadi leo saa 7:45 mchana mvua hizo hazijaleta madhara yoyote.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Mussa Taibu amesema hakuna taarifa zozote za madhara alizopokea kutoka mipaka ya wilaya hiyo.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, Amon Kakwale amesema, “hadi sasa sijapata taarifa za madhara lakini hata nyie vyombo vya habari ni chanzo cha kukusanya taarifa, kama kuna mahali nimesikia mtusaidie."

Mwananchi limepita maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na kushuhudia baadhi ya mabasi yaendayo haraka (Dart) yakiondoka katika kituo chake eneo la Jangwani ambalo hujaa maji.

Katika eneo la Jangwani hadi leo saa 6 mchana maji yalikuwa yamejaa na kuanza kupita juu ya daraja hali iliyosababisha magari kupita taratibu na kusababisha foleni kutokana na kuanza kutumika kwa barabara moja kwa magari yanayokwenda na kutoka katikati ya Jiji.

Advertisement

Barabara nyingine iliyojaa maji ni ya Umoja wa Mataifa eneo la Upanga na magari kulazimika kuchepuka pembeni ya barabara hiyo.

 

 

Advertisement