Mwandishi wa habari Lobulu afariki dunia

Sunday October 6 2019

 

By Filbert Rweyemamu, Mwananchi [email protected]

Arusha. Mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania, William Lobulu amefariki dunia leo Jumapili Oktoba 6, 2019 nyumbani kwake Sanawari, mjini Arusha.

Enzi za uhai wake Lobulu alimiliki  gazeti la kila wiki la The Arusha Times na pia amewahi kuwa mkufunzi katika Chuo cha Uandishi wa Habari (TSJ) miaka ya 1980 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha, Claud Gwandu amesema taratibu za mazishi zitatolewa baadaye.

Lobulu alianza uandishi wa habari mwaka 1976 mara baada ya kuhitimu shahada ya kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kufanya kazi Shirika la Habari Tanzania (Shihata).

Advertisement