Mwandishi wa habari Marin Hassan Marin afariki dunia

Muktasari:

Mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania, Marin Hassan Marin amefariki dunia leo asubuhi Aprili Mosi, 2020 jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania, Marin Hassan Marin amefariki dunia leo asubuhi Aprili Mosi, 2020 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi mkuu wa TBC, Dk Ayoub Rioba amethibitisha kifo cha mtangazaji huyo.

“Taarifa kuhusu mipango ya mazishi zitatangaza baadaye, “ amesema mtangazaji wa shirika hilo, Gabriel Zakaria wakati akizungumzia kifo cha Marin.

Katika taarifa ya kifo hicho iliyosomwa na Zakaria akimnukuu Dk Rioba, alionyesha kipande cha video ya  Machi 30, 2020 inayoonyesha tukio lililowahusisha wafanyakazi wa shirika hilo akiwemo Marin ambaye pia alizungumza kuhusu tukio hilo.

 

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi