Mwenye maambukizi ya corona ajifungua salama

Uganda. Mmoja wa wagonjwa waliothibitika kupata mamabukizi ya virusi vya corona nchini Uganda amejifungua mtoto mwenye afya njema.

Mama huyo mwenye miaka 22 kutokea Kyengera wilayani Mwakiso iliripotiwa alipata alipata maambukizi kutoka kwa mume wake aliyerejea nchini humo kutokea Dubai.

Mkuu Mkuu wa Hospitali ya Entebbe, Dk Moses Muwonge amesema mgonjwa huyo amejifungua mtoto wa kike Jumamosi saa 8 mchana.

”Mgonjwa alijifungua leo mchana (jana) kwa njia ya upasuaji na wote mama na mtoto wana afya nzuri kabisa” amesema Muwonge

Hadi Ijumaa Aprili 3 Uganda ilikuwa na wagonjwa 48 wenye maambukizi ya virusi vya corona