VIDEO:Mwili wa Robert Mugabe wawasili Zimbabwe

Wednesday September 11 2019

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe,Ndege wa Harare,

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Harare. Mwili wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe umewasili Uwanja wa Ndege wa Harare nchini humo leo Jumatano Septemba 11, 2019 ukitokea Singapore.

Mugabe  alifariki dunia Septemba 6, 2019 nchini humo alikokuwa akipatiwa matibabu ikiwa ni takribani miaka miwili tangu alipoondolewa madarakani.

Viongozi wa nchi hiyo wakiongozwa na Rais, Emmerson Mnangagwa, familia na wananchi zaidi ya 2,000 wamejitokeza uwanjani hapo kuupokea mwili wa mwanamapinduzi huyo aliyeliongoza Taifa hilo miaka 37.

Mwili wake utapelekwa nyumbani kwake na kesho Alhamisi Septemba 12, 2019 utaagwa katika uwanja wa Rufaro wenye uwezo wa kuingiza watu 35,000. Uwanja huo ulitumika wakati akiapishwa Aprili, 1980.

Rais wa China, Xi Jinping, rais wa zamani wa Quba, Raul Castrol na marais mbalimbali wa Afrika ni miongoni mwa watakaoudhuria mazishi Jumamosi Septemba 14, 2019.


Advertisement

Advertisement