NDANI YA BOKSI: Muziki wetu si Bongo Fleva tena-2

Saturday August 24 2019

 

Enzi zile Bongo Fleva ilionekana ni muziki wa watoto wa kishua, ilionekana kama wao ndio wenye muziki huo, kwa kuwa wao ndio walioonekana kuutawala, sasa watoto wa Uswahilini nao wakaanza kuwatolea macho, wakawa na maono ya mbali kwamba muziki unaweza kuwaondoa kwenye ujinga na umaskini.

Kina Sugu mapema kabisa miaka ya 1998 wakaanza kufunga mikanda, kina Profesa Jay wakaweka kando ajira zao Tigo. Sasa muziki ukawa mali ya watoto wa Uswahilini na kuwa kitu kigeni kwa watoto wa kishua. Hii ndiyo iliyofanya Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’ na vijana wenzake wa East Coast Team. Wapate wakati mgumu sana kila walipokutana na watoto wa TMK kina Juma Nature.

Kwa imani kuwa Bongo Fleva ni ya watoto wa uswahilini. Wasio na uwezo wala elimu ya kutosha. Watoto wa Upanga wakawa kama wanaimbia sifa tu na siyo sehemu ya maisha. Licha ya uwepo wa wanamuziki kutoka kwenye familia ‘wezeshi’ (wakishua). Kama kina Mike Tee, ambao walienda studio kurekodi ngoma wakiwa ‘wanapushi’ benzi. Unique Sisters watoto wa Mzee Kipozi. Hawakuweza kuimeza idadi kubwa ya watoto wa Uswahilini, walioutolea macho muziki kama ndo ‘Mastazi na Piechidii’ yao.

Leo hii hali imekuwa tofauti. Unapomuona Vanessa Mdee akienda ‘lesi’ kwenye muziki. Ndipo unagundua watoto wa Uswahilini wamefanya mpaka wazee wa ‘ushuani’ waruhusu watoto wao wafanye muziki.

Baada ya kuona kuna maisha ndani ya muziki. Hata Davido ni wa kishua, ujeuri wake tu. Wazazi hawakutaka afanye muziki.

Mambo yamebadilika. Kama kina Vanessa Mdee watoto wa kishua wameamua kutafuta pesa kwa kukata nyonga majukwaani.

Advertisement

Kusoma Makala yote tafadhali usikose gazeti la Leo jumamosi Agosti 24, 2019

Advertisement