NEC wazungumzia ratiba feki uchaguzi mkuu 2020

Muktasari:

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (Nec) imekanusha kutoa ratiba ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kama inavyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikielezwa kuwa  ratiba itaanza Aprili 28.

Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (Nec) imekanusha kutoa ratiba ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kama inavyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikielezwa kuwa  ratiba itaanza Aprili 28.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa uchaguzi wa Nec,  Dk Wilson Charles imewataka wananchi kuwa watulivu na kupuuza taarifa potofu zinazotolewa na watu wenye nia ovu.

Kulingana na taarifa hiyo tume itatoa ratiba ya uchaguzi mkuu muda utakapowadia kulingana na matakwa ya kisheria.

Kwa mujibu wa Nec, sheria ya uchaguzi inaielekeza kutangaza tarehe ya uchaguzi mara baada ya kuvunjwa kwa Bunge.

“Kwa kuwa Bunge halijavunjwa, tume haijatoa wala kutangaza ratiba yoyote ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020,” imeeleza taarifa hiyo.