Nandy: Nilikuwa na ndoto kufanya kazi na Sauti Sol

Tuesday September 10 2019

 

By Elizabeth Edward, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Siku chache baada ya kuachia wimbo wa Kiza Kinene kwa kushirikiana na  kundi la Sauti Sol la nchini Kenya, msanii Nandy amesema alikuwa  na ndoto kufanya kazi na kundi  hilo.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram leo Jumanne Septemba 10, 2019, Nandy amevunja ukimya na kueleza namna alivyokuwa akiota kufanya kazi na Sauti Sol.

Nandy ameweka kipande cha video kinachomuonyesha akiwa kwenye shindano na  msanii wa Sauti Sol, Bien akionekana kumsifia.

“Ilikuwa ndoto yangu kufanya kazi na kundi la Sauti Sol nakumbuka kipindi hiki nawaza nikishinda niimbe na wewe,” amesema Nandy.

Wimbo wa Kizakinene unaonekana kufanya vizuri kwenye vituo vya redio na televisheni huku kwenye youtube ukifikisha watazamaji zaidi ya 700,000 ndani ya siku tatu tangu video itoke.

Wakati wimbo huo ukifanya vizuri bado Bugana ambao Nandy ameshirikiana na  Billnass nao ukifanya vyema na kufikisha watazamaji milioni moja ndani ya wiki moja.

Advertisement

 


Advertisement