Ndugai ataka wasaniiwa sanaa za ufundi wasajiliwe

Monday May 13 2019

By Rachel Chibwete, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Spika wa Bunge Job Ndugai amewataka watendaji wa kata na mitaa kuwatambua wasanii wa sanaa za ufundi waliopo kwenye maeneo yao ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana nchini.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Mei 13, 2019 kwenye hotuba yake iliyosomwa na Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga kwenye ufunguzi wa semina ya mradi wa utambuzi wa wasanii wa Sanaa za Ufundi Tanzania (TACIP) kwa watendaji wa kata na mitaa wa jiji la Dodoma.

Spika amesema watendaji hao ndiyo wenye watu kwa hiyo ni jukumu lao kuwatambua na kuwasajili ili waweze kujulikana na kuzitumia fursa zinazopatikana ili kuwanufaisha kiuchumi.

“Kundi hili la wasanii wa sanaa za ufundi ni kundi kubwa kuliko hata lile la wasanii wa muziki na wa filamu lakini hawasikiki wala kutupigia kelele,” amesema Ndugai.

Advertisement