Ozil afunguka kuhusu kutemwa Ligi Kuu

kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil

Muktasari:

Kiungo huyo Mjerumani hajapangwa katika kikosi cha Arsenal tangu mwezi Machi na sasa ameachwa katika kikosi cha wachezaji 25 watakaocheza mechi za Ligi Kuu ya soka England.

London, England. Baada ya kuachwa katika kikosi cha wachezaji 25 wa Ligi Kuu ya England, kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil amesema anatia shaka utii wa wachezaji wengine katika kikosi hicho na kwamba ataendelea kutumia 'sauti yake dhidi ya vitendo visivyo vya kibinadamu na kwa ajili ya haki'.

Mchezaji huyo hajapangwa katika mechi za vigogo hao wa London tangu Machi na kocha wake, Mikel Arteta ameamua kuwa nyota huyo wa Ujerumani si mchezaji mzuri kuweza kupata nafasi katika kikosi chake.

Ozil, ambaye analipwa zaidi ya dola 456,000 kwa wiki na klabu hiyo, ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa katika Ligi Kuu ya Soka ya England.

Hali inaonekana si nzuri kati ya Ozil na kocha wake na mapema mwezi huu, mchezaji huyo aliyekuwa katika kikosi cha Ujerumani kilichotwaa Kombe la Dunia nchini Brazil, aliiambia klabu yake kuwa yuko tayari kumlipa mshahara mshsrehesjai wa Arsenal (mascot) maarufu kwa jina la Gunnersaurus, ili kulinda ajira yake klabuni.

Here is the Mesut Ozil statement in full:

“Huu ni ujumbe mgumu kuuandika kwa mashabiki wa Arsenal kwamba nimecheza kwa miaka michache iliyopita. Nimefedheheka sana na ukweli kwamba sijasajiliwa kucheza Ligi Kuu kwa sasa. Wakati wa kusaini mkataba wangu mpya mwaka 2018, niliahidi kuwa mtiifu na mwaminifu kwa klabu nayoipenda, Arsenal, na inaniumiza hili halifanywa hivi (na upande wa pili). Kama nilivyoona, utiifu ni mgumu kuja siku hizi. Wakati wote nimejitahidi kuendelea kuwa na imani wiki baada ya wiki kwamba labda nafasi ya kurejea katika timu itakuja hivi karibuni.

“Kabla ya mapumziko ya ufgonjwa wa virusi vya corona, nilikuw ana furaha hasa na maendeleo chini ya kocha mpya Mikel Arteta – tumekuwa katika hali nzuri na nilisema kiwango changu kilikuwa kizuri," alisema Mjerumani huyo.

"Lakini baadaye mambo yalibadilika, kwa mara nyingine sikuruhusiwa kucheza soka Arsenal. Nitasema nini zaidi? Bado London ni kama nyumbani, bado nmina marafiki wengi wazuri katika timu hii, na bado najiona ninakubalika na mashabiki wa klabu hii. Liwalo na liwe, nitaendelea kupigania nafasi yangu na sitakubali kuachia msimu wangu wa nane uishe namna hii. Naweza kuwaahidi kuwa huu uamuzi mgumu hautabadili lolote katika akili yangu – nitaendelea kufanya mazoezi kadri niwezavyo na popote itakapowezekana nitatumia sauti yangu dhidi ya udhalilishaji wa binadamu na kutetea haki.”

Mkataba wa Ozil unaisha majiora ya joto ya mwaka 2021na sasa anaonekana kama anajiandaa kuondoka Arsenal kwa sababu Arteta haondoki na ameipandisha timu kiwango chake.