Profesa Kabudi ataja changamoto zinazoikabili dunia

Muktasari:

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Profesa Palamagamba Kabudi ametaja changamoto zinazoikabili dunia katika utekelezaji wa malengo endelevu kuwa ni pamoja na matukio ya usalama ya mabadiliko ya tabianchi.

Dodoma. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Profesa Palamagamba Kabudi ametaja changamoto zinazoikabili dunia katika utekelezaji wa malengo endelevu kuwa ni pamoja na matukio ya usalama ya mabadiliko ya tabianchi.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Oktoba 24, 2019 mjini Dodoma katika maadhimisho ya miaka 74 ya Umoja wa Mataifa (UN).

Amesema katika baadhi ya mataifa kumekuwa na matukio mbalimbali  ya ugaidi, vita ambayo inatakiwa kutatuliwa.

“Tunapoadhimisha mikaa 74 ya UN dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali za ugaidi, vita, migogoro na mabadiliko ya tabianchi. Jambo hili linarudisha nyumba utelekezaji wa  maendeleo,” amesema Kabudi.

Mwakilishi wa Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA),  Jacqueline Mahon amesema UN ina sababu ya kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwahudumia wakimbizi kutoka nchi jirani, kuitaka kuendelea na moyo huo licha ya changamoto mbalimbali zilizopo.