VIDEO: Raia wa Poland adakwa akituhumiwa kulima bangi Tanzania

Muktasari:

Kikosi kazi cha Mamlaka  ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa  za Kulenya Tanzania kikiongozwa na Kaimu Kamishina Jenerali, James Kaji, kimemkamata raia wa Poland, Damian Sanikowsiki (40) kwa tuhuma za kulima na kumiliki shamba la bangi katika eneo la Himo wilaya ya Moshi mkoa Kilimanjaro.

Moshi. Kikosi cha kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini Tanzania, kimemkamata raia wa  Poland, Damian Sanikowsiki (40) kwa tuhuma za kulima shamba la bangi eneo la Njiapanda ya Himo, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio leo Jumapili Februari 9,2020, kaimu kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo, James Kaji amesema mtuhumiwa alikamatwa jana Jumamosi baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwapo kwa shamba hilo.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamishina Jenerali, mtuhumiwa amekamatwa pamoja na watu wengine na kwamba mahojiano na watuhumiwa yanaendelea ikiwamo kukusanya vielelezo.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa pia akiwa na bangi iliyoongezewa thamani kwa kuiweka kwenye keki na nyingine iliyosindikwa mfano wa asali ambayo hutumiwa na wateja wa ndani na nje ya Tanzania.