Rais Magufuli amsifia Waziri Bashungwa

Monday September 16 2019

 

By Emmanuel Mtengwa, Mwananchi

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amempongeza Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa kwa utendaji wake wa kazi.

Akizungumza leo Jumatatu Septemba 16, 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha mabomba cha Pipe Line Limited kilichopo Vingunguti amesema wizara hiyo inaenda vizuri baada ya kumteua waziri Bashungwa.

“Napenda nisema ingawaje wakati mwingine ukimsifia mtu ni vibaya, Wizara ya Viwanda sasa hivi walau inaelekea kuzuri na mimi nakusifu Bashungwa (Waziri wa Viwanda na Biashara).”

Amesema baada ya Serikali kuamua kununua korosho zilikaa kwa muda mrefu bila kupata soko lakini Bashungwa alipoteuliwa alianza kutafuta soko.

 “Mfano mmoja tu ambao umejiridhisha, Serikali tuliamua kununua korosho miezi iliyopita, tumekaa nazo bila kutafutwa mnunuzi, nilipomteua tu huyu (Bashungwa) akaanza kutafuta wanunuzi.

“Mpaka sasa hivi korosho za Sh130 bilioni zimeshanunuliwa na zishasombwa na meli mbili na kuna meli nyingine ipo nayo inapakia.

Advertisement

“Kwa hiyo unaona angalau yupo mtu anaamua kuliko ambaye hawezi kuamua,  mimi sipendi mtendaji ambaye ananichelewesha, nataka matokeo,” amesema Rais Magufuli.

Advertisement