Rais Magufuli atua Chato

Muktasari:

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema Rais John Magufuli leo Jumamosi Machi 28,2020 amewasili Chato mkoani Geita akitokea jijini Dodoma.

 

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumamosi Machi 28,2020 amewasili Wilaya ya Chato mkoani Geita akitokea jijini Dodoma.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania, Gerson Msigwa imesema Rais Magufuli ametua katika uwanja wa ndege wa Chato kisha kwenda nyumbani kwake katika kitongoji cha Lubambangwe, Kijiji cha Mlimani wilayani Chato.