Samia amtahadharisha RC mpya Morogoro

Sunday September 22 2019

 

By Bakari Kiango, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewapongeza viongozi wote walioteuliwa na kuapisha huku akimtahadhalisha mkuu mpya wa mkoa wa Morogoro, Loata Sanare akisema mkoa huo una changamoto kubwa ya mgogoro ya ardhi ya wakulima na wafugaji

Ametoa kauli leo Jumapili Septemba 22, 2019 wakati wa hafla ya kuwaapisha baadhi ya viongozi walioteuliwa Septemba 20,2019 akiwamo Sanare aliyechukua nafasi ya Dk Stephen Kebwe.

Katika hafla ya hiyo, Samia amesema watendaji waliotoka ofisi moja kwenda nyingine ni mabadiliko ya kawaida huku akiwa na matumaini watatumia uzoefu kwenye sehemu mpya walizopewa.

Samia ametumia nafasi hiyo kwa kumpa tahadhari Sinare kwa kusema

“unakwenda pale wafugaji wataona mfugaji mwenzetu yupo hapa na kuna kesi nyingi sana. Usiangalie ng’ombe wa Ole lengai  hakikisha unatenda haki kwa wakulima na wafugaji.”

“Uwepo wako watakuwa wakipiga vigelegele na kusema zile lori za saa nane usiku za kumimina ng’ombe Morogoro sasa zitakuwa huru. Una mtihani mkubwa Morogoro, kasimamie vizuri,” amesema Samia.

Advertisement

Advertisement