Samsung kuja na betri zinazodumu na chaji muda mrefu

Saturday August 24 2019

 

Samsung wanapambana kupunguza gharama za utengenezaji wa betri mpya zitakazokuwa zinadumu na chaji kuliko zinazotumika sasa.

Teknolojia hiyo mpya waliyokuja nayo inafanya betri ya simu iweze kudumu muda mrefu kwa matumizi mengi baada ya kuchaji ukilinganisha na ubora wa betri zinazotengenezwa kwa teknolojia inayotumika sasa.

Samsung walitambulisha rasmi ugunduzi wa teknolojia yao mwaka 2004 ila hadi sasa wanafanya utafiti zaidi kuhakikisha ubora, usalama na uwezo wa kutengeneza betri hizo.

Teknolojia hiyo ina gharama kubwa kwa kila utengenezaji wa betri moja ukilinganisha na betri zinazotumika sasa.

Kampuni hiyo imebainisha kuwa utafiti huo upo katika hatua za mwisho kabla ya betri hizo kuanza kutumika.

Advertisement