Shibuda atumia misemo, nahau kuuzungumzia uchaguzi serikali za mitaa

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa John Shibuda akizungumza na wanahabari baada ya kupata taarifa ya ripoti ya uangalizi wa uchaguzi wa Serikali ya mtaa iliyofanywa na  asasi ya Tafeyoco

Muktasari:

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya siasa John Shibuda kasoro zilizojitokeza katika mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa ni fursa ya kujenga mwamko kusahihisha hitilafu hizo ili zisijitokeze tena katika chaguzi zijazo.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Tanzania, John Shibuda amesema kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni fursa ya kujenga mwamko mpya wa kusahihisha hitilafu hizo ili zisitendeke kwenye chaguzi za msimu ujao.

Shibuda ambaye ni kiongozi wa chama cha Ada Tadea ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Desemba 6, 2019  wakati akipokea taarifa ya ripoti ya uangalizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji iliyofanywa na asasi ya kirai ya Tafeyoco.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Novemba 24, 2019 vyama vya upinzani vya Chadema, CUF, ACT- Wazalendo, UPDP na Chaumma vilisusia mchakato huo kwa kile walichodai kutoridhishwa na mwenendo wake huku vyama vya NRA, DP, AAFP na TLP vikishiriki.

Miongoni mwa mambo yaliyojitokeza katika mchakato ni asilimia kubwa ya wagombea wa vyama vya upinzani kuenguliwa baada ya kukosa sifa huku baadhi ya waliochukua fomu wakijikuta wakishindwa kurudisha baada ya ofisi za Serikali kufungwa.

Akizungumza kwa mtindo wa nahau na methali, Shibuda  amewaambia wanahabari  ukweli uliopo Taifa lina fadhaa ya mgogoro wa kuhusu kuwepo kwa kasoro ya uborongwaji na uparaganishwaji wa ndiyo na wa siyo kwa kanuni za uchaguzi huo.

"Kwa hiyo sasa, msemo wa hakuna chema kisicho na kasoro umetua vyema katika uchaguzi wa serikali za mtaa wa mwaka huu. Kwa kutambua kwamba leo kusema uchaguzi wa serikali za mitaa haukuwa na kasoro ni sawa na kujaribu kuficha kaa la moto kwenye mfuko wa kanzu.”

"Kwa kutambua wadau wa vyama vya siasa na umma wa wakereketwa wa masuala haya wana fikra ya taftishi za kusaka suluhu, suluhu inayohitajika ni kujenga utulivu wa fikra kwa uwazaji wa kuelekea katika dira ya msimu wa duru za siasa za uchaguzi wa mwakani," amesema Shibuda.

Shibuda amekubali kuyapokea maoni ya Tafeyoco akisema ni sehemu ya taarifa itakayoondoa ukomo na ulegevu kwa mambo ya mtu mwenye taarifa za kutaka kujua asiyoyajua.

"Msema kweli ni mpenzi wa Mungu sasa tukiri ndani ya jamii yetu pana kuna gumzo za kimya kimya na mijadala ya uwazi ya kuhusu fikra za kutangatanga za hoja ya kutaka kujua endapo kuna uongo au ukweli unaogusa changamoto za Serikali za mtaa," amesema Shibuda.

Awali, akiwasilisha ripoti ya uangalizi wa uchaguzi huo, mkurugenzi Mtendaji wa Tafeyoco, Elvice Makumbo amesema miongoni mwa mambo waliyoyabaini ni baadhi ya vyama vya siasa kushinda kushirikiana na wagombea wa