Si kila mwenye ualbino ana saratani ya ngozi

Saturday August 24 2019

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dodoma.  Shirika la kimataifa la Under The Same Sun limesema baadhi ya watu wenye ualbino wamekuwa wakipewa rufaa katika hospitali kubwa kwa kudhaniwa wana saratani ya ngozi jambo ambalo hubainika kuwa si kweli baada ya vipimo.

Kutokana na hali hiyo, afisa sheria wa shirika hilo,  Maduhu William amewaomba  waganga wakuu wa mikoa na wilaya kuwakumbusha watendaji wao ili wawe wanafanya uchunguzi wa kina kwa walemavu hao kabla ya kuwapatia rufaa.

Akizungumza na wadau wa afya wakiwamo  waganga wakuu wa mikoa na wilaya mkoani Dodoma,  Maduhu amesema baada ya kupimwa baadhi yao huonekana kuwa na vidonda vya kawaida lakini si saratani.

Maduhu ameeleza kuwa ni vizuri kukawa na utaratibu wa kuwapima saratani walau mara moja kwa mwezi ili kuwasaidia waweze kukabiliana na saratani.

Under The Same Sun ni miongoni mwa mashirika yanayoshiriki kikao hicho kinachoenda sambamba na  maonesho ya huduma za afya, utetezi na vifaa tiba.

Advertisement