Siku ya kupiga kura hakuna usafiri wa majini Zanzibar

Muktasari:

Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) imetangaza kusitisha safari za vyombo vya usafiri wa baharini siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28, 2020.

 

Dar es Salaam. Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) imetangaza kusitisha safari za vyombo vya usafiri wa baharini siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28, 2020.

Taarifa iliyotolewa kwa umma na mamlaka hiyo siku mbili zilizopita inaeleza, “Siku ya Jumatano Oktoba 28, 2020 ni siku maalumu ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Tanzania,”

“Kutokana na umuhimu wa siku hiyo, mamlaka inakujulisha kuwa imesitisha safari zote za boti na meli za abiria na mizigo ili kutoa fursa kwa wananchi waliojiandikisha kupiga kura waweze kukamilisha zoezi hilo kikamilifu.”

Aprili 25,mwaka jana ZMA ilisitisha usafiri huo kutokana na kuwapo tahadhari ya kutokea kimbunga nchini kabla ya kurejea hapo baadaye.