Sugu ataka matokeo ya urais kupingwa mahakamani

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 bungeni jijini Dodoma leo. Picha na Anthony Siame

Muktasari:

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ ametaka sheria za uchaguzi zibadilishwe ili matokeo ya urais kupingwa mahakamani kama ilivyo kwa ubunge.

Dodoma. Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ ametaka sheria za uchaguzi zibadilishwe ili matokeo ya urais kupingwa mahakamani kama ilivyo kwa ubunge.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Aprili 2, 2020 katika mjadala wa bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2020/21.

Sugu ambaye pia ni mwanamuziki amesema mbali na matokeo kupingwa, uwepo wa tume huru ya uchaguzi utafanya uchaguzi uwe huru na haki.

“Mbeya hamjawahi kunipa ushindi kwenye silver plate, mwaka 2010 alikufa mtu mmoja kwa ajili ya kulinda kura, uchaguzi wa mwaka 2015 walemavu watatu hadi leo bado nawahudumia.”

“Kwa hiyo tunataka tume huru yenye uwezo wa kuchagua wasimamizi wake na watumishi wake yenyewe ila isiteuliwe,” amesema Sugu.