Breaking News

Taasisi yadai shule chanzo watoto kuwa na tabia zisizofaa

Saturday October 17 2020

By Habel Chidawali, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Wazazi wameshauriwa kuwa makini katika uchaguzi wa shule wanazopeleka watoto wao ili kuwajengea misingi ya kitaaluma na kitamaduni.

Wito huo umetolewa leo Jumamosi Oktoba 17, 2020 na mkurugenzi wa taasisi ya The Islamic Foundation,  Ibrahim Twaha Ibrahim katika sherehe za kuhitimu elimu ya msingi kwa shule ya Zamzam Islamic ya jijini Dodoma.

Ibrahim alisema katika kuchagua shule, kazi ni kwa wazazi kwani watoto kwa sehemu yao huwa bado wadogo ambao hawana uwezo wa kujua.

Kiongozi huyo alisema majina ya shule yamekuwa yakiwafanya wazazi waamini kuwa shule fulani ni nzuri lakini mwisho wake watoto hutumbukia kwenye tabia zisizofaa na kufanya elimu waliyoisoma kuonekana haina maana tena.

"Hili la kusema tunakwenda shule za ‘international’  bila kufuatilia misingi na mienendo ya shule, msichague taaluma pekee bali angalieni hata tabia na mambo yanayosimamiwa kwenye shule hizo," amesema Ibrahim.

Jumla ya wanafunzi 34 wamefanyiwa sherehe hizo baada ya kumaliza elimu ya msingi.

Advertisement

 

Advertisement