Takukuru yaokoa Sh50.8 bilioni

Wednesday April 15 2020

By Sharon Sauwa, Mwananchi

Dodoma. Jumla Sh 50.8 bilioni zimeokolewa kutokana na operesheni mbalimbali za uchunguzi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo uliofanyika nchini katika mwaka wa fedha 2019/2020.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo Jumatano Aprili 15, 2020 wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake bungeni.

Amesema Sh6.7 bilioni ni fedha taslimu, Sh11.2 bilioni ni thamani ya mali zilizotaifishwa ambazo ni nyumba tatu na viwanja vinne, Sh3 0bilioni ziliokolewa baada ya uchunguzi kufanyika na kubaini mzabuni aliongeza bei kwenye huduma aliyotoa serikalini na Sh2.9 bilioni zilidhibitiwa na kurejeshwa kwa wananchi.

Aidha, amesema fedha na mali zilizowekewa zuio kusubiri kukamilika kwa utaratibu wa kisheria wa utaifishaji ni Sh7.0 bilioni, Dola za Marekani 5.26 milioni, magari 14 yenye thamani ya Sh635 milioni, nyumba 14 zenye thamani ya Sh13.0 bilioni na nyumba moja yenye thamani ya Dola 410 za Marekani.

Advertisement