VIDEO: Tanzania kujumuishwa nchi zitakazowekewa vikwazo na Marekani

Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk Inmi Patterson

Muktasari:

Tanzania imetajwa miongoni mwa nchi saba ambazo raia wake watakumbana na vikwazo watakapotaka kwenda Marekani.

Dar es Salaam. Tanzania imetajwa miongoni mwa nchi saba ambazo raia wake watakumbana na vikwazo watakapotaka kwenda Marekani.

Leo Jumatano Januari 22, 2020 kaimu balozi wa Marekani, Dk Inmi Patterson akihojiwa na Redio Clouds amethibitisha suala hilo baada ya jana jioni taarifa za Tanzania na nchi hizo kuwekewa vikwazo kuanza kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Nchi nyingine zilizotajwa ni Belarus, Eritrea, Kyrgyzstan, Myanmar, Nigeria na Sudan.

Katika mahojiano na gazeti la Wall Street, Rais wa Marekani, Donald Trump ambaye yupo kwenye kongamano la uchumi linaloendelea huko Dacos, Switzerland hakutaja nchi hizo kwa kueleza taarifa rasmi itatoka mwezi ujao.

Taarifa ya mtandao wa Politico imeeleza nchi hizo zinaweza kufahamika Jumatatu Januari 27, 2020.

Juni 28, 2018 mahakama ya juu ya Marekani iliidhinisha zuio la nchi tano zenye itikadi ya Kiislam ambazo ni Somalia, Libya, Iran, Syria na Yemen.