Tanzania mwenyeji mkutano CPA

Thursday August 22 2019

Rais wa Zanzibar Dk Mohamed Shein, Chama cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola ,

 

Dodoma. Rais wa Zanzibar Dk Mohamed  Shein atafungua mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA).

Akizungumza leo Alhamisi Agosti 22,  2019 Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema zaidi ya maspika 20 kutoka nchi wanachama wamethibitisha kushiriki katika mkutano huo utakaoanza Agosti 31 na kumalizika Septemba 5, 2019.

Amesema mkutano huo utakaofanyika Zanzibar una faida mbalimbali ikiwemo utalii na wafanyabiashara nchini watapata nafasi ya kutoa huduma kwenye mkutano.


Advertisement