Tume ya Ulaya yaidhinisha uuzaji chanjo ya Ebola

Ubelgiji. Tume ya Ulaya imeidhinisha uuzaji wa chanjo ya kwanza ya ugonjwa wa Ebola. 

Dawa hiyo imekuwa ikitengezwa tangu kuzuka kwa ugonjwa huo katika eneo la Magharibi mwa Afrika mwaka 2014 na imekuwa wakipewa watu wanaokabiliwa na kiwango kikubwa cha maambukizi.

Wagonjwa hao ni pamoja na wafanyakazi wa huduma za afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akizungumza jana Jumatatu Novemba 11, nchini Ubeligi, Kamishna wa Afya, Vytenis Andriukaitis alisema kuwa kupata chanjo dhidi ya virusi hivyo hatari haraka iwezekanavyo ni kipaumbele kwa jamii ya kimataifa.

Andriukaitis amesema baada ya majaribio yaliyofanywa na wakala wa dawa wa Ulaya (Ema) itairuhusu kampuni kubwa ya kuuza dawa Marekani,. Merck kuanza kuisambaza kwa jina la Everbo.

Tangu kuanza kwa mlipuko wa karibuni wa ugonjwa huo nchini DRC na kuua watu 2,150 kuanzia Agosti 2018, zaidi ya watu 236,000 wamepata chanjo hiyo.

Kati ya watu hao ni, watumishi 60,000 wa afya. Chanjo hiyo imeanza kutumika kinyume cha taratibu kwa kuitoa kabla ya kibali katika mazingira ya dharura.

Imejaribiwa kwa watu 16,000 katika tiba za afya barani Afrika, Ulaya na Marekani na kuonekana iko sawasawa. Takwimu za ziada zinakusanywa.