Tundu Lissu ahofia usalama wake kurejea Tanzania

Muktasari:

Mdhamini wa Tundu Lissu, Ibrahim Ahmed, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa mshtakiwa huyo amepona, ila ameshindwa kurudi nchini Tanzania kwa kuhofia usalama wake.

Mdhamini wa Tundu Lissu, Ibrahim Ahmed, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa mshtakiwa huyo amepona, ila ameshindwa kurudi nchini Tanzania kwa kuhofia usalama wake.

Ahmed ameieleza mahakama hiyo, leo Alhamisi Novemba 21,2019, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati wa kesi ya uchochezi inayomkabili mshtakiwa huyo na wenzake watatu ilipoitwa.