UREMBO: Mabadiliko ya homoni kila mwezi husababisha chunusi

Licha ya kufanya vitu kadha wa kadha kulinda ngozi isiharibike, kuna sababu za kimaumbile ikiwamo mabadiliko ya homoni ambayo huifanya ngozi kubadilika na wakati mwingine kupata chunusi.

Hili hutokea ka baadhi ya wanawake kila mwezi wanapokuwa kwenye hedhi. Ukijua jinsi ya kusimamia tarehe unazopata hedhi itakuwa rahisi kuilinda ngozi na uso wako na chunusi wakati wa mabadiliko hayo.

Unachotakiwa kufanya ukiona tarehe zinakaribia ni kukanda uso kwa mvuke. Yaani chemsha maji yaweke kwenye chombo kipana kama beseni kisha jifunike nguo nyepesi ili kupata mvuke, hakikisha hayana moto sana ili kuepuka kubabuka.

Unaweza pia kufanya hivyo kwa mashine maalumu ya mvuke, zinapatikana saluni za kike na za kiume.

Vitu vingine unavyoweza kufanya katika kipindi hicho ni kuhakikisha unaosha uso mara mbili kwa sabuni zisizo na mafuta, usipake vipodozi vyenye mafuta na usilale na vipodozi usoni.