Ulega: Kuosha mifugo ni lazima si hiari

Monday February 17 2020

By Filbert Rweyemamu, Mwananchi [email protected]

Arusha. Naibu Waziri wa Mifugo nchini Tanzania, Abdallah Ulega amesema utaratibu wa kuosha mifugo kwa ajili ya kuikinga na kupe ni lazima.

Ulega amesema hayo leo Jumatatu Februari 17, 2020  wakati akifungua kongamano la wadau wa mifugo lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) kutoa matokeo ya utafiti magonjwa ya mifugo hasa minyoo bapa.

Amesema wakati Serikali inajikita kuboresha afya ya mifugo ili kuwawezesha wafugaji kupata tija ni muhimu wafugaji wote kuosha mifugo yao kwenye majosho yaliyo katika maeneo yao mara mbili kwa mwezi.

"Awali kupeleka mifugo kwenye majosho ilikua hiari sasa hivi tumeweka utaratibu wizarani ambao unalazimisha mfugaji kuwapeleka kwenye josho kulingana na utaratibu uliowekwa," amesema Ulega

Amesema mwaka 2019/2020 Serikali imetumia Sh450 milioni kununua lita 12,550 za dawa kwaajili ya majosho  1,733 nchi nzima.

Advertisement