VIDEO: Ulimwengu, Himid washuhudia Samatta akibeba jiko Dar

Thursday October 10 2019

 

By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Straika wa Genk na Taifa Stars, Mbwana Samatta amefunga ndoa leo usiku Alhamisi Agosti 10, 2019 na Neima Mgange huku akishuhudiwa na marafiki zake wa karibu, Thomas Ulimwengu na Himid Mao.

Mbali na mastaa hao ambao wamekipiga na Samatta, lakini wakazi wa mtaa wa Kichangani huko Mtoni Kijichi wamejawa na furaha baada nahodha huyo wa Stars kuoa mtaani kwao.

Wakazi wengi wamefurahi nyumbani kwa Mzee Mgange wakitaka kumuona Samatta laivu hasa baada ya hivi karibuni kuweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kukipiga Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli.

Mwanaspoti ambalo liko bega kwa bega kwenye tukio hilo kukupasha kila kinachoendelea limeshughudia nyomi ya wakazi hao ambao wamefurika wakimsubiri Samatta.


Advertisement