Umeshawahi kujiuliza ubora wa dawa zinazouzwa mitandaoni

Muktasari:

Matarajio ya wanandoa wanapoanza kuishi pamoja ni kupata watoto ili waanze kujenga familia.

Dar es Salaam. Matarajio ya wanandoa wanapoanza kuishi pamoja ni kupata watoto ili waanze kujenga familia.

Hata hivyo, matarajio hayo hugeuka kitendawili kisichokuwa na majibu iwapo mwanamke anachelewa kushika mimba.

Siku hizi changamoto hiyo imekuwa fursa kwa baadhi ya watu ambao wanadai kuwasaidia wanaokumbana na changamoto ya kutopata ujauzito au wenye matatizo yoyote ya kiafya kwa kuwauzia dawa zinazotibu tatizo hilo. dawa hizo zinauzwa katika mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook.

Wauzaji hao wanatumia akaunti mbalimbali za watu au taasisi kutangaza biashara hizo na mtu anayehitaji huambiwa awasiliane nao ili wampelekee alipo bila kujua undani wa tatizo la mhusika.

Mfano, changamoto ya uzazi unashindwa kupata ujauzito na umehangaika kwa muda mrefu? Sasa tutafute (anataja mawasiliano yake) tuna suluhisho la changamoto zote za uzazi. Tupigie simu au WhatAsap

Mwingine ni ile akaunti iliyoweka tangazo likieleza maumivu wakati wa tendo la ndoa ni dalili mojawapo ya PID, “kwa tiba na ushauri piga (namba za simu ziliwekwa)” huku likisema mteja anaweza kufikiwa popote alipo.

 

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumapili Agosti 25, 2019.