Uturuki yauwa wanajeshi wawili wa Syria

Muktasari:

Yatupa kombora katika kituo cha jeshi kilichopo Kaskazini Mashariki ambacho kilikuwa na wanajeshi ya Syria.

Uturuki. Wanajeshi wawili wa nchini Syria wameuawa baada ya kombora la jeshi la Uturuki kuanguka katika eneo lao.

Mauaji hayo yalifanyika jana Jumatano Oktoba 16, katika kituo kilichopo Kaskazini Mashariki ambacho kilikuwa na wanajeshi ya Syria.

Kufuatia hatua hiyo, Rais wa Urusi, Vladimir Putin amezungumza kwa kwa njia ya simu na mwenzake wa Uturuki Recep Erdogan na kumwalika kiongozi huyo kufanya ziara haraka nchini Urusi.

Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya Putin, ni kwamba mualiko huo umekubaliwa na atakwenda nchini Urusi katika siku zijazo kwa ziara ya kikazi.

Taarifa inasema pande zote mbili zimekubaliana uhitaji wa kuepusha makabiliano kati ya vikosi vya Uturuki na Syria.

Katika mawasiliano hayo Rais Putin alionesha wasiwasi wake kwamba huenda magaidi wakatumia mwanya huo kujiingiza katika mataifa hayo katika kipindi hiki ambacho serikali ya Uturuki inayashambulia maeneo ya Wakurd huko kaskazini mwa Syria.

Nae mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa (EU), nchini Syria, Geir Pedersen amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya kigeni wa Syria, Walid al-Moualem mjini damascus na kuzusha suala la mapambano ya Uturuki kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.