VIDEO: Balozi Iddi aeleza alivyokaa karantini Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais  Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi

Muktasari:

Makamu wa Pili wa Rais  Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amewataka wananchi kuzingatia kukaa karantini wanapoingia Tanzania kutoka nchi zenye maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Zanzibar. Makamu wa Pili wa Rais  Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amewataka wananchi kuzingatia kukaa karantini wanapoingia Tanzania kutoka nchi zenye maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Hivi karibuni Balozi Iddi  alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Cuba, baada ya kurejea Zanzibar alikaa karantini kwa siku 14.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Alhamisi Aprili 2, 2020 baada ya kumaliza siku hizo 14, amesema kila msafiri ana wajibu wa kukaa karantini huku akibainisha jinsi wataalamu wa afya walivyomshauri kuongeza siku nyingine saba.

 “Kukaa karantini sio adhabu ni jambo linalotusaidia sisi mfano mimi na timu yangu tumetoka Cuba hadi Zanzibar tumepita nchi mbalimbali zilizoathirika na ugonjwa huu,” amesema.

Balozi Idd amewataka watu kuvaa barakoa na kunawa mikono kujikinga na maambukizi huku akitoa tahadhari watu kukusanyika, hasa kwenye misiba kwamba ni jambo la kuchukua tahadhari.